Skip to content Skip to main navigation Skip to footer

BURIANI STELLA MACHOCHO WANGAMA

Bunge la Kaunti ya Taita Taveta limepokea kwa masikitiko makubwa habari za kufariki kwa Stella Machocho ambaye ni mkewe Mjumbe wa Wadi ya Wusi-Kishamba, Mhe. Dancun Wangama.

Kifo cha Stella ni pigo kubwa kwa mumewe, jamii yake na wote waliomfahamu na kumpenda.

Kwa niaba ya Bunge letu la Kaunti, ninatuma rambirambi zetu za dhati kwa Mhe. Wangama na wapendwa wake wote.
Tungependa kukuhakishia kuwa tutakushika mkono na kusimama nawe wakati huu mgumu wa majonzi.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze pahali pema peponi roho ya Stellah, na kuwapa nguvu na faraja wote aliowaacha.

Mhe. Anselm Mwadime Chao
Kaimu Spika wa Bunge la Kaunti

Back to top